Acts 8:5-10

5 aFilipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
6Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema. 7 cPepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele na wengi waliopooza na viwete wakaponywa. 8Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo.

Simoni Mchawi

9 dBasi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu, 10 enao watu wote wakubwa kwa wadogo wakamsikiliza na kumaka, wakisema “Mtu huyu ndiye uweza wa Mungu ujulikanao kama ‘Uweza Mkuu.’ ”
Copyright information for SwhKC